Idara ya Kiswahili Yaandaa Webina Kusherehekea Miaka 50 Tangu Chuo Kikuu Cha Nairobi Kianzishwe
Mnamo tarehe 2, Disemba, 2020, Idara ya Kiswahili iliandaa webina spesheli kusherehekea miaka 50 tangu chuo kikuu cha Nairobi kilipoanzishwa rasmi. Mada kuu ya webina hio ilikuwa, “Kiswahili Ulimwenguni.”
Webina hio ya kufana, ilihudhuria na watu wa tajriba mbali mbali miongoni mwao wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi, Wahadhiri na wasomi kutoka pande tofauti tofauti ulimwenguni ikiwemo, Poland, Ghana, Uganda, Tanzania, Mariakani na Uchina.